Bank ya Dunia (WB) wametoa list ya nchi ambazo zinakuwa haraka kiuchumi
mwaka 2017 huku nchi za Afrika na Asia zikionekana kushika kasi katika
kukuza uchumi wake kutokana na kukua kwa biashara na miundombinu.
Katika list hii Ethiopia inakamata nafasi ya kwanza ambapo uchumi wake umekua kwa 8.3% huku Tanzania ikitajwa
miongoni mwa nchi 10 ikikamata nafasi ya tano uchumi wake ukikua kwa 7.2%
huku uchumi wa Djibouti ukikua kwa 7% licha ya kukabiliwa na ukame
mkubwa katika nchi hiyo